Monday, December 12, 2011

Tottenham walambishwa mchanga

Stoke 2 - 1 Tottenham

Emmanuel Adebayor aliifungia Tottenham penalti
Rekodi ya Tottenham kupata ushindi katika mechi 11 mfululizo ilivunjwa na timu ya Stoke City siku ya Jumapili baada ya mchezaji wa zamani wa Tottenham Matthew Etherington kuingiza magoli mawili dhidi ya moja la Spurs.
Etherington aliingiza goli la kwanza katika dakika ya 13 na baada ya dakika 30 akaongeza la pili.
Tottenham walipata goli lao moja kupitia kwa mkwaju wa penalti lililofungwa na katika dakika ya 62.
Tottenham walijitahidi ili wapate kusawazisha lakini matumaini yao yakafifia baada ya Younes Kaboul kuonyeshwa kadi nyekundu.
Spurs pia hawakufurahishwa na baadhi ya maamuzi yaliyotolewa na refarii Chris Foy.
Tottenham sasa wana alama 31 ikiwa ni alama tano nyuma ya Manchester United walio kwenye nafasi ya pili.

Sunderland 2- 1 Blackburn.

Katika matokeo mengine ya ligi kuu nchini England Sunderland walipata ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Blackburn Rovers.
Ushindi huu umempa kocha mpya wa Sunderland Martin O'Neill mwanzo mzuri.
Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa O'Neille kama msimamizi wa Sunderland tangu achukue uongozi baada ya Steve Bruce kupigwa kalamu.
Ushindi huu ambao ni wao wa tatu tangu ligi ianze umeipandisha Sunderland hadi nafasi ya 16

No comments:

Post a Comment