Thursday, January 3, 2013

Wazanzibari kuweni wamoja



Miwenyekiti wa Baraza la katiba Zanzibar,Pr Abdull Shariff
Miwenyekiti wa Baraza la katiba Zanzibar,Pr Abdull Shariff

Mwenyekiti wa baraza la katiba zanzibar Pr Abdul Sharif amesema kuwa kero zitokanazo na  muungano uliopo baina ya tanganyika na zanzibar kumesababishwa na ukiukwaji wa hati halisi inayobainisha uundwaji wa muungano huu.
Hayo ameyasema leo wakati alipokuwa akizungumza katika kongamano lililoandaliwa na baraza la katiba zanzibar lilofanyika katika ukumbi wa tawi la Chuo Kikuu cha Taifa  Zanzibar (SUZA) uliopo Beit el Raas ambapo kulihudhuriwa na baadhi ya wanafunzi  wa vyuo vikuu mbalimbali pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti ya zanzibar waliofika katika kongamano hilo ikiwa ni miendelezo ya makongamano ya kuwaelimisha wananchi juu ya suala zima la mustakabali wa nchi.
Pr Abdul amebainisha kuwa serikali ya muungano wa haikua na nia ya kuiimarisha na kuiletea maendeleo bali ilikua na nia ya kuindoshea mamalaka zanzibar na kuwa sehemu ya tanganyika ndio maana wakaamua kuyachota madaraka ya smz na kuingiza katika madaraka ya serikali ya muungano wa tanzanzia na kuvuruga mgawanyo wa madaraka kati ya kati ya serikali hizi mbili uliokubaliwa 1964.
Aidha amefahamisha kuwa kutokana na ibara ya 64 ya katiba ya tanzania ya 1977ilitoa nafasi kwa serikali ya tanzania kuweza kujiongezea madaraka kinyume na mgawanyo wa madaraka kati ya serikali hizi mbili kwani sheria hii ilipitishwa kama sheria za kawaida bila ya kuzingatia theluthi mbili za wabunge wa zanzibar na hapo ndipo wakafanikiwa kupitisha zaidi ya sheria 30 ikiwemo bahari kuu iliozua malumbano hivi karibuni.
Na kwa upande wa bwana Almasi kutoka zanzibar youthn  forum amesisitiza kuwepo muungano wa mkataba ambao utawapa wazanzibar uhuru wa kuweza kujiamulia wanayotaka kwa lengo la kuendeleza uhusiano bila ya kuwepo kero.

No comments:

Post a Comment