Wednesday, January 11, 2012

Karume ndiye muasisi wa serikali ya umoja Z’bar- Moyo


 


MWASISI wa Mapinduzi ya Zanzibar na mwanaharakati katika vyama vya wafanyakazi vilivochangia kuleta mapinduzi hayo, Hassan Nassoro Moyo anakumbuka mengi kuhusu tukio hilo.
Anasema sema Abeid Amani Karume (hayati)  aliunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama iliyopo sasa ya CCM na CUF kwa lengo la kuleta mshikamano na kuondosha mawazo ya chuki na uhasama.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Moyo anasema kuwa kabla ya mapinduzi, chuki na uhasama ikiwamo watu kugawanywa katika makabila na rangi vilitawala kwa kiasi kikubwa.
 
Tulipofanya mapinduzi… Mzee Karume aliunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuvishirikisha vyama vya siasa ikiwamo Umma Party, anasema.
Anasema kwa upande wa Umma Party viongozi waliochaguliwa kuunda serikali alikuwa pamoja na Abrahman Babu na Khamis Ameir na baadaye walikuja kina Ali Sultani pamoja na Badawi.
Moyo anasema kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa kunatokana na ilani (manifesto) ya chama cha Afro Shirazi ambacho kilitamka bayana kwamba kikipata madaraka kitaunda serikali itakayowashirikisha wananchi wote wa visiwa vya Unguja na Pemba .
 
Anasema kuundwa kwa serikali hiyo kwa kiasi kikubwa ilisaidia kuleta mshikamano wa wananchi na viongozi ambacho chuki zilizokuwapo awali zikaanza kutoweka hatua kwa hatua.
Serikali ya umoja wa kitaifa ya chini ya Afro Shirazi ilifanikiwa kuvunja matabaka na watu wote kuwa kitu kimoja huku hakuna mtu mmoja kujiona yeye bora zaidi,anasema.
Naye kiongozi aliyepata kuwa Waziri wa Elimu na baadaye Waziri wa Afya, Ali Sultani anasema Karume alikuwa kiongozi jasiri mwenye nia ya dhati ya kuona wananchi wake wanaondokana na madhila na unyanyasaji wa aina yoyote ile.
 
Niliteuliwa waziri wa elimu ambapo nilipewa jukumu la kuhakikisha kila baada ya kilometer mbili kunakuwa na shule kwa lengo la kufupisha masafa ya watoto kutafuta elimu,anasema.
Aidha, anasema hayati Karume hakupenda kuona watu wanaonewa bure na kunyanyaswa ambapo katika mwaka 1968 alianzisha ujenzi wa makazi ya watu wasiojiweza yaliyoko Sebleni, Zanzibar kwa lengo la kuona wazee wanapata hifadhi nzuri wakati wanapoishiwa nguvu.
Hatua hiyo ilikwenda sambamba na serikali kubinafsisha ardhi iliyokuwa ikimilikiwa na watu wachache wakiwemo ukoo wa Kisultani.
 
Aidha, Serikali ya Afro Shirazi ilitangaza elimu bure kwa wananchi wote ikiwamo watoto wa wakulima na wakwezi ambao kabla ya hapo walishindwa kupata huduma za elimu zilizokuwa na vikwazo vingi.
Kutokana na nia hiyo madhubuti ya rais huyo wa kwanza waa Zanzibar ya kuwaweka pamoja Wazanzibari wote ndio leo unaona serikali hii ya awamu ya saba nayo imekuja  na mfumo ule ambao ulikuwa unamuumiza kichwa Karume, anasema Moyo.
 
Katika kuendeleza fikra za mapinduzi, Rais wa awamu ya Saba, Dk Ali Mohammed Shein  ameendelea kufuata nyo za waasisi wa Mapinduzi kwa hivi karibuni akiweka jiwe la Msingi la Shule ya Uzini alisema, “Hakuna mtu yeyote atakaye kosa nafasi ya kusoma na tena bila ya malipo.”
Mzee Moyo ambaye wakati mapinduzi yanatokea  alikuwa Katibu mkuu wa Vyama vya Wafanyakazi ambavyo vilirishiki kikamilifu katika kuleta mapinduzi ya hayo ya mwaka 1964.
 
Vyama vya wafanyakazi vilikuwa madhubuti tofauti na leo, anasema mzee huyo.
Sambamba na hilo Mzee Moyo hukusita kuutambua uhuru uliopatiakna mwaka 1963 Disemba.
Alisema hule ulikuwa uhuru hallali wa Zanzibar kwani vyama vyote vilitia saini ya makubaliano huko London Uengereza katika Jumba la Lancaster, London ambapo yeye alienda kama mwangalizi.
Baada ya hapo wanyonge waliukataa uhuru hule na kusema kuwa uhuru hule wa mwarabu na baadae kuanda Mapinduzi.

Mapinduzi yale hayakuja tu hivihivi bali yalipangwa muda mrefu na tarehe 12 Januari ilikuwa kilele tu,anafahamisha.
Lakini kutokana na sheria za nchi leo ndio huwezi kusema hule ndio uhuru kutokana .
Mzee Moyo alisema leo unayoyaona yote ni yale matunda ya Mapinduzi amayo ndio yalikuwa na lengo la kupata umoja wa Wazanzibari.
Leo Wazanzibari wote wanaishi kwa amani bila hofu na hii yote ni kutokana na malengo mya Mapinduzi ya kumkomboa mwananchi wake.
 
Tulifanya Mapinduzi ili kuondoa matabaka katika jamii ambayo kwa kiasi kikubwa tumefanuikiwa na hali munaiyona nyote alisema moyo huku anacheke.
Alifahamisha kwamba leo kila kikchochoiro unaona skuli  tena ya sekondari haya ndio malengo ya Mapinduzi.
Leo  tunaadhimisha miaka 48 ya Mapinduzi kwa kujivunia maendeleo makubwa yaliopo katika visiwa vyetu vyote
Lengo la Karume alikusudia kuondoa masafa ya vijana kufuata masoamo na leo hii si zaidi ya kilomitqa mbili mtoto amefika skuli.
Tujipigieni makofi wanangu haya ni mambo makubwa yalifanywa na viongozi wetu, anachekesha

No comments:

Post a Comment