Friday, January 20, 2012

Zanzibar yapinga Tanzania kudai eneo zaidi la mpaka wa bahari kuu


 

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar sasa wanasema ombi la serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa kuomba nyongeza ya mpaka katika Bahari ya Hindi ni kuipokonya Zanzibar haki yake.

 
Ombi hilo tayari limeshawasilishwa katika  Umoja wa Mataifa, New York, na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi wa Tanzania, Professa Anna Tibaijuka, akitaka kilomita 150 zaidi za bahari.
Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa aliyeliibua suala hilo kwenye Baraza la Wawakilishi hapo juzi, sasa anakusudia kuwasilisha hoja binafsi ya dharura kwenye Baraza hilo hapo Jumatatu, akitaka lazima kuwepo na mazungumzo ya kuamua nani anamiliki nini kati ya Tanzania na Zanzibar kabla ya ombi hilo kuwasilishwa katika  Umoja huo.
Amina Abubakar amezungumza na Ismail Jussa kuhusiana na msimamo huo.
Mahojiano: Amina Abubakar/Ismail Jussa

No comments:

Post a Comment