Wednesday, March 28, 2012

Anayechezea amani ya Zanzibar alaaniwe


Mwenyekiti wa Chama Cha Wanaanchi (CUF) Professa Ibrahim Haruna Lipumba akifungua vifurushi alivyoandaliwa kwa ajili ya kuwasha rasharasha kama ishara ya kukaribisha Zanzibar katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti kabla ya kuhudhuria mamia ya wanachama wa chama hicho
Mwenyekiti wa taifa wa chama cha wananchi (CUF) Prof Ibrahim Haruna Lipumba amewataka wazanzibari kulinda umoja uliyoopo visiwani na kwamba yoyote anayetumiwa kuwagawa wazanzibari, anafaa kutengwa na kulaaniwa. Lipumba alitowa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara uliyoanyika viwanja vya Kibanda-Maiti mjini hapa, huku akishangaliwa na mamia ya wafuasi na wapenzi wa chama hicho. mkutano ambao ulihudhuriwa na mamia ya watu mbali mbali wakiwemo wa vyama vyengine.
“Mzanzibari anayechezea amani, ni lazima tuelewe kuwa hatutakii mema,” Prof Lipumba alisema huku hotuba yake ikikatishwa mara kwa mara na ushangiliaji wa watu waliyohudhuriwa mkutano huo. na kuongeza kwamba.
“Anayeleta chokochoko kwa wazanzibar, anayetaka kuwagawa wazanzibari huyo anafaa kulaamiwa” alisema Profesa Lipumba na kuungwa mkono na mashabiki hao,
Lipumba alisema wazanzibari wanapaswa kuzingatia kwa umakini wapi wametoka na wamefanya juhudi gani katika kuhakikisha amani inadumu hivyo katu wasirudi nyuma na kusiistiza kwamba amani iliyopatikana imepatikana kwa gharama kubwa na wakati mwingi hivyo inapaswa kulindwa na kila mmoja.
Huu ulikuwa mkutano wa kwanza wa Profesa kufanyika katika kisiwa cha Unguja tangu kutrudi kutoka Marikani March 11 mwaka ambapo alipokelewa na watu wengi wakiongozwa na wakaazi wa Dar es Salaam.
Hotuba ya Lipumba ilionekana wazi kuwafurahisha watu waliyojitokeza katika mkutano huo kwani wakati ambapo baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiongozwa na Hamad Rashid Mohamed wanavutana na uongozi wa chama hicho.
“Wazanzibari wanakila sababu ya kuhakikisha kuwa CUF kinakuwa ngangari na kumlaani yoyote atakaejaribu kuwatenganisha wananchi na kuvuruga umoja uliyekuwepo,” Lipumba.
Bila kumtaja kwa jina, pia makamo mwenyekiti wa CUF Bw Machano Khamis Ali alisema kuwa “Kibwetere (labda akimaanisha Hamad Rashid na kundi lake) anatarajiwa kupata usajili wa muda chama chake siku ya jumatatu, halafu aje kufanya mkutano wa hadhara Zanzibar, Tanga, na Pemba. Kibwetere na anasema atahakikisha anakiua cuf, je ataweza!”
Akizungumzia safari yake ya miezi mitano nchini Marikani, Lipumba alisema alikutakana na watafiti na watalam wenzake wa Uchumi ambao waliangalia swala la tatizo la umasikini barani afrika na rasilimali zilizoopo.
“Tumebahatika kuwa na rasili mali nyingi katika bara la afrika, lakini bado watu wetu wengi ni maskini. Hi inatokana na mipango mibaya, ambapo wanachi hawanufaiki na mali na mapato ya serikali,” alisema.
Alisema kwamba hivi sasa nchini Tanzania harakati zinaendelea za kutafuta gesi asilia na mafuta, ambapo baadhi ya maeneo mfano Mtwara tarayi Gesi asilia imegundulikana, na maeneo mengine ya Pemba matumaini ya upatikanaji mafuta ni makubwa.
Hata lipumba alitahadharisha kuwa rasilimali ya Gesi na Mafuta isiwe ni chanzo cha migogoro, “rasilimali hizi ni neema, lakini inaweza kuwa ni chanzo cha migororo mikubwa kama ilivyo Nigeria…na Sudani.”
Profesa lipumba alisema kuwa ili kuepusha mgogoro, ni lazima kwanza serikali kuandaa utaratibu bora wa kugawana mapato, ambapo kila raia hasa maskini waliyowengi wahisi kuwa wananufaika na rasilimali hizo. “wachambuzi wanasema ili kuleta utawala bora katika nchi zenye gesi na mafuta ni kuweka utaratibu bora,” alisema.
“Mfano, utaratibu unaweza kuwa mapato ya milioni moja dola za kimarikani zinazopatikana kwa mwaka kutokana na mauzo ya mafuta, sehemu fulani, zigawe kwa kila familia. Au kinachopatikana kila mwezi,” alisema lipumba.
Alisema neema ya Gesi na Mafuta inakuja, Zanzibar inahaki ya kudai haki zake ndani ya muungano kwani Zanzibar na Tanzania ni nchi mbili zikiwa na haki sawa ndani ya muungano. “Zanzibar ni nchi, bara ni nchi zilizoungana. Lazima ktk muungano tuweze kuheshimiana.”
Alisema “Zanzibar inahitaji kutafuta haki zake, na wakati wa kutafuta haki ni huu wa kuandika katiba…na sote tushiriki katika katiba.”
Alisema ni lazima Katiba ya nchi ijayo itamke wazi mgawanyo wa mapato ya mfuta. Ni muhimu kuweka utaratibu mapema. Nigeria wameshindwa tangu mwaka 2002 kuweka utaratibu mzuri, Watanzania na wazanzibari ni vizuri kuweka mipango mizuri.
Mapema katika mkutano huo, katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad alisema kwamba mapokezi ya Prof Lipumba aliporudi kutoka Marikani ni ushahidi tosha kuwa CUF hakijafa Bara, na kwamba chama kipo imara.
“Nataka kuwatoa wasiwasi wanachama wa CUF kuwa kwamba cuf haijafa bara, mapokezi ya Mwenyekiti Dar es Salaam ni dhihirisho kuwa CUF ni hai. Baadhi ya watu wamelinganisha Mapokezi hayo na mapokezi ya nelson Mandela alipotoka jela. Lakini ni zaidi ya hao,” alisema Seif.

No comments:

Post a Comment