KARUME APASUKA DODOMA
MIONGONI MWA DONDOO YA HUTUBA YA MWENYEKITI MSTAAFU WA CCM AMANI KARUME HUKO DODOMA
AKIZUNGUMZIA KUHUSU HALI YA KISIASA ZANZIBAR AMESEMA INARIDHISHA TENA SANA ISIPOKUWA KUNA MAMBO MADOGO MADOGO YANAYOFANYWA NA WANAHARAKATI NA SIWANASIASA NA AMEZIPONGEZA SERIKALI ZOTE MBILI KWA HATUWA WALIZOZICHUKUWA KUDUMISHA AMANI, NA ANAKUBALIANA MIA KWA MIA KUIUNGA MKONO SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA KWANI NI MWANA WAO WALIOMZAAA WENYEWE KWAHIO HATUNA BUDI KUIUNGA MKONO SERIKALI HIO.
AMESEMA KUA SASA IWEJE LEO HII BAADHI YA WENZETU WAWE NA WASIWASI NA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA TULIOIUNDA WENYEWE NA SISI TUKIWA MIONGONI MWA TULICHUKUA ZAMANA YA KUIDUMISHA SERIKALI HII NA DHAMANA YA MWISHO IPO KWA WAZANZIBARI WENYEWE KWANI NDIO WALIOPIGA KURA YA MAONI NA AMEWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUIUNGA MKONO SERIKALI HIO VYENGINEVYO TUTAMPA TABU TAIS SHEIN
AKIZUNGUMZA KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA AMESEMA KUWA WATANZANIA WOTE WATOE MAWAZO YAOjJUU YA KATIBA MPYA KWANI NDIO INAVOTAKIWA NA KATIKA UTOWAJI WA MAWAZO LAZIMA TUHESHIMIANE NA WENGINE KWANI ANAJUA WAZI KUWA KUNA WENGINE WAKO WANAOTAKA SERIKALI YA WENGINE ILIOPO IENDELEE NA WENGINE WANATAKA SERIKALI TATU SASA CHA MUHIMU NI KUJIFUNZA KUVUMILIANA TU
AIDHA AMEULIZA NA KWANINI IWE NONGWA PALE IPOTUOKEA BAADHI WATU KUTOA MAONI YAO IKAWA NI TOFAUTI NA WENZAO LINALOMSHANGAZA YEYE KUITANA MAJINA YA AJABU AJABU ETI KWA SABABU YA MAONI NA KUSEMA KUWA WATU ZANZIBAR WANATISHANA ETI WANATAKA KUMREJESHA SULTAN AMESEMA KUWA SUALA HILO KWA SASA HALIPO KABISA KWANAZA SULTAN AMESHAKUFA NA KUULIZA KUWA HIVI WANACHIHAWAIJUI NA KUISOMA KATIBA YA ZANZIBAR AMBAYO INAONESHA WAZI KUWA NI JAMUHURI
No comments:
Post a Comment