Thursday, December 29, 2011

Mgeja azungumzia dhana ya kujivua gamba CCM

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja amesema maudhui ya kujivua gamba
yaliyoasisiwa na Mwenyekiti wao wa Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ni kuhakikisha chama kinarejea kwenye uasilia wake.

Amefafanua kuwa uasilia wa CCM ni umoja, upendo, mshikamano, kukosoana na kujisahihisha
pamoja na kusimamia maadili na miiko ya uongozi, jambo ambalo ndani ya Chama Cha Mapinduzi, limeanza kupotea kidogo kidogo kwa kasi kubwa.

Mgeja aliyasema hayo katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM
wilayani Meatu hivi karibuni wakati alipozungumza na wazee, viongozi na wanachama katika
ziara yake ya kuwashukuru wananchi kuipigia kura Serikali ya CCM ingawa ilipoteza ubunge
katika jimbo hilo.

Akifuatana na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, Salum
Khamis maarufu kwa jina la Mbuzi, Mwenyekiti huyo alisema falsafa hiyo ni nzuri pindi kila
mwanachama akiielewa vizuri maudhui yake hasa katika kipindi hiki ambacho CCM inakabiliwa na changamoto za ndani na nje ya chama.

Mgeja alibainisha kuwa CCM uasilia wake ni viongozi wake kuanzia ngazi ya Tawi ni kujielekeza
kutatua kero na kushughulikia kwa uadilifu miradi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kwamba inakabiliwa na changamoto zinazowakabili wananchi katika maisha yao ya kila siku.

Aidha, aliwashauri viongozi na wanachama wa CCM waondokane na kuitafsiri dhana hii
kinyume cha maudhui yake halisi, tafsiri ambazo zimesababisha migawanyiko na kupandikiza chuki na kuleta mitafaruku ya ndani ya chama badala ya kujenga inatengeneza nyufa kubwa zisizo na maslahi ya chama.

Kwa upande wake, Mbuzi aliwashukuru wananchi wa Meatu kwa kumpa ushirikiano kipindi
cha mwaka 2005 hadi 2010 katika kufanikisha masuala ya maendeleo hadi kuiwezesha Wilaya ya Meatu kuwa ya mfano katika wilaya za Mkoa wa Shinyanga katika sekta za elimu, miundomHamis Mgeja binu ya barabara na michezo.

No comments:

Post a Comment