Thursday, January 12, 2012

MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 48 YA MAPINDUZI ZANZIBAR



Kikosi cha Polisi wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.
Kikosi cha Wanajeshi waenda kwa miguu, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni wa rasmi.

Kikosi cha kutuliza ghasia FFU, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa Mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wakipita kwa maandamano na mabango mbele ya Jukwaa Kuu.
.Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaani Uwanja wa Amani katika Sherehe hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment