Thursday, January 12, 2012

Video yalaaniwa: Wanajeshi "Wamarekani" wakikojolea maiti wa Taleban




Rais wa Afghanistan Hamid Karzai leo amelaani vitendo vinavyoonekana kwenye video ambapo wanajeshi wanaosadikiwa kuwa wa jeshi la Marekani wanaonekana wakikojolea maiti wa Taleban.

Rais Karzai amekitaja kitendo hicho kuwa "kisicho cha kibinadamu hata kidogo" ("completely inhumane") na kulitaka jeshi la Marekani kuwaadhibu waliohusika na kitendo hicho.

Uongozi wa Jeshi la Marekani jana ulisema kuwa unachunguza video hiyo iliyowekwa kwenye mtandao jamii wa video "YouTube" ili kuthibitisha (authenticity) kabla ya kuchukua hatua.

Jeshi linaloongozwa na NATO limesema nchini Afghanistan limesema, "This disrespectful act is inexplicable and not in keeping with the high moral standards we expect of coalition forces."

Uongozi wa "International Security Assistance Force" nao umesema, "appear to have been conducted by a small group of U.S. individuals, who apparently are no longer serving in Afghanistan."

Seneta wa Arizona, Marekani, John McCain, ambaye ni veterani wa vita vya Vietnam amesema, "makes me so sad" na kuongeza,  taswira ya jeshi la Marekani imechafuliwa na "a handful of obviously undisciplined people." na kumalizia katika kipindi cha  leo cha "CBS This Morning," kuwa, "There should be an investigation and these young people should be punished."

Jana, baraza la "Islamic-American Relations" lenye makao yake makuu jijini Washington, lililaani video hiyo na kutuma barua kwa njia ya fax kwa Wwaziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta ikisema, "We condemn this apparent desecration of the dead as a violation of our nation's military regulations and of international laws of war prohibiting such disgusting and immoral actions,..." "If verified as authentic, the video shows behavior that is totally unbecoming of American military personnel and that could ultimately endanger other soldiers and civilians,...".

Uongozi wa kikosi cha maji cha ulinzi makao makuu nchini Marekani, Pentagon umesema: "The actions portrayed are not consistent with our core values and are not indicative of the character of the Marines in our Corps. This matter will be fully investigated."

Msemaji wake Lt. Col. Stewart Upton, akaongeza, "Allegations of Marines not doing the right thing in regard to dead Taliban insurgents are very serious and, if proven, represent a failure to adhere to the high standards expected of American military personnel."

Bado haijatambulika bayana ni nani alichukua video ya kitendo hicho na ni nani aliyeipakia mtandaoni.

No comments:

Post a Comment