Msemaji wa Jeshi la nchi hiyo Meja Emmanuel Chirchir amesema kundi al Shabaab lenye mafungamano na kundi la kigaidi la al Qaeda ambalo kwa hivi sasa lipo upande wa kusini wa Gaebahare lilikuwa likipanga kuyashambulia majeshi ya Kenya na Somalia katika miji miwili ya karibu ambayo ilidhibitiwa na vikosi vya Kenya wiki hii.
Akizungumza na Shirika la Habari la Uingereza, Reuters, msemaji huyo aliongeza kusema shambulio hilo ni pigo kubwa kwa wapiganaji hao waliokuwa wakipanga kushambulia wanajeshi wa Kenya waliokuwepo katika miji ya Fafadun na Elade.
Kenya ilipelekea majeshi yake katika ardhi ya nchi jirani ya Somalia Oktoba mwaka jana baada ya kutokea matukio ya utekaji nyara na mashumbilo katika maeneo ya mipakani yaliyofanywa na kundi la al Shabaab ambayo yalitishia kuzorotesha sekta ya Utalii ya Kenya.
Kundi la al Shabaab limekuwa kitisho kikubwa cha usalama katika eneo la Afrika Mashariki, jambo lililoufanya Umoja wa Afrika wenye kikosi cha ulinzi wa amani huko katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, kutanua mamlaka ya ulinzi wa amani na kuomba Umoja wa Mataifa kuliongezea nguvu jeshi hilo kufikia wanajeshi 18,000.
Awali Kenya ilisema inadhibiti miji ya Fafadun na Elade iliyopo kusini magharibi mwa jimbo la Gedo, baada ya kutokea mapigano yaliyosababisha vifo vya wapiganaji watatu wa al Shabab
No comments:
Post a Comment