Hali ni mbaya katika barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiishi hapo, japokuwa serikali imekuwa ikiwaambia hawatakiwa mkujenga katika eneo hilo kutokana na madhara yanayoweza kutokea endapo mvua zitanyesha,Lakini hali ndivyo ilivyo kwa sasa, ambapo katika eneo hilo maji yamefurika nyumba zinaelea kwenye maji na barabara hiyo imefunikwa na maji na kusababisha vyombo vya usalama kuifunga, hivyo kukata mawasiliano kati ya Kariakoo na mjini maeneo na Magomeni. Kutokana na nvua ambayo imenyesha siku mbili mfurulizo jijini Dar es salaam Watu ni wengi katika eneo hilo lakini pia kutokana na ubishi, kunawatu wamekuwa wakizolewa na maji kwa sababu ya kulazimisha kuvuka, wakati maji hayo yanaenda kwa kasi kubwa, baadhi ya watu wamekuwa wakiokolewa na vikosi vya uokoaji na wanapelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, kama wanavyoonekana wakina mama hawa katika picha wakipelekwa kwenye gari baada ya kuokolewa kwenye maji.
Akina mama hawa wakilia baada ya kuokolewa kwenye maji hapa walikuwa wakielekea kupanda gari tayari kwa kuwapeleka hospitali ya muhimbili kwa uangalizi zaidi wa afya zao.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kushoto amekuwepo pia katika tukio hilo la uokoaji, hapa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanausalama.
Hapa ni mahali ambapo pamewekwa uzio ili kuzuia watu kuvuka ng'ambo yaani uapnde wa pili. Baadhi ya watu wakiokooa vitu vyao na kuviweka kando ya barabara ya Morogoro.
Hawa wajapan wanaofanya kazi katika kampuni ya Kajima yenye ofisi zake hapo Jangwani ambayo nayo imevamiwa na maji na kuharibu vitu mbalimbali huku maji yakiwazingira baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwa wakiokolewa na vikosi wa uokozi.
No comments:
Post a Comment