Thursday, December 29, 2011

MAAJABU NA KWELI: MTI UNAOUWA WANANDOA..HAUKATIKI WALA HAUHAMISHIKI


Eneo hili linaitwa Wawili Wapendanao na hapa ni Karatu Barabara yanapopita mabasi yaendayo Mwanza, ni maarufu kutokana na huu mti unaoonekana pichani ambao umeshindikana kwa namna yeyote kuuondoa ama kuukata mahala hapa.
Wenyeji wa maeneo haya wameuambia Mtandao wa Sufianimafoto kuwa, hata wajenzi wa Barabara hii walijaribu kutaka kuukata bila mafanikio kwani haukatiki wala haung'oki pamoja na kwamba walijaribu kila njia ikiwa ni pamoja na kufuata mila za kiswahili zilizoelekeza kuukata mti huo usiku wa manane bila mafanikio.
Aidha imeelezwa kuwa mti huo pia umekuwa maarufu zaidi kutokana na kutokea ajali za mara kwa mara katika mti huo na kuua watu, ambapo tayari zimekwishatokea ajali kadhaa ikiwa ni pamoja na ajali mbili za wanandoa waliotoka kufunga pingu za maisha na wakati wakirejea kuelekea ukumbili safari yao ikaishia katika mti huu na hiyo ilikuwa ni mwaka jana tu, wakati mwaka juzi pia ilitokea ajali kama hiyo ya kusikitisha mahala hapa.

No comments:

Post a Comment